Mbali na Shamte washtakiwa wengine ni Ofisa Mkuu wa Fedha, Raphael Onyango, Mhasibu Said Ally, Ofisa Masoko, Noel Chacha, Msimamzi wa Mtandao, Tinisha Max na Mkuu wa Takwimu wa Biashara wa kampuni hiyo, Vishno Konreddy.
Mwendesha Mashtaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Theophil Mutakyawa, aliyekuwa akisaidiana na Wakili Jackline Nyantori na Wakili Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Johanes Kalungura, walidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo siku tofauti kati ya Mei 20 mwaka jana na Januari mwaka huu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, ilidaiwa kuwa, siku ya tukio washtakiwa hao kwa nia ya kujipatia faida binafsi walitoza kiwango cha chini zaidi ya kile kilichowekwa na serikali cha dola 25 senti (USD 25 Cents), kwa dakika na kushindwa kulipa kiasi cha dola milioni 3,836,861.99 kwa TCRA.Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washtakiwa kwa kutoza tozo chini ya kiwango walishindwa kulipa mapato yaliyokuwa yakitokana na mawasiliano ya kimataifa ya simu zilizokuwa zikiingia na kusababisha serikali kupata hasara ya dola za Kimarekani 3,836,861.99.
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama Kuu au mpaka Mkurugenzi wa Mashataka (DPP) atoe kibali cha kesi hiyo kusikilizwa mahakamani hapo.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Mwijage aliiahirisha hadi Januari 29, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment