Sheikh huyo amesema kitendo hicho hakikubaliki na hakiendani na haki za binadamu, kwani kila mtu ana haki ya kuishi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Sheikh Jalala alisema kesi ya Sheikh Nimr haikuendeshwa kwa uadilifu na kwamba lengo la unyongaji wa wanaharakati wa kisiasa na kidini nchini Saudia ni kutaka kuzima sauti za ukosoaji dhidi ya utawala wa nchi hiyo, hususani wanavyofanyiwa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Alisema Sheikh Nimr hakuwaita watu kwenye harakati za kubeba silaha wala kuwaita watu kwenye mipango ya siri na kupanga njama za kufanya maovu, bali alisimama na kujishughulisha na kukemea na kukosoa kwa namna ya wazi na kuamrisha mema kutendeka na kukataza maovu kutokana sheria za kidini.
Alisema licha ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kuendelea Saudi Arabia, bado kuna wasiwasi unaotokana na madai ya kiraia na malalamiko yanayoongezeka kuhusiana na ubaguzi na ukanyagaji wa haki za raia pamoja na kukosekana utawala wa kidemokrasia.
Alisema licha ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kuendelea Saudi Arabia, bado kuna wasiwasi unaotokana na madai ya kiraia na malalamiko yanayoongezeka kuhusiana na ubaguzi na ukanyagaji wa haki za raia pamoja na kukosekana utawala wa kidemokrasia.
Naye Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, alitoa taarifa kueleza kwamba kunyongwa kwa Sheikh Nimr, kumezusha wasiwasi mkubwa kuhusu uhuru wa maoni na kuheshimiwa haki za kisiasa na kiraia nchini humo.
Januari 2, mwaka huu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia Arabia ilitoa taarifa kuwa Sheikh Nimr Baqir Al-Nimr pamoja na watu wengine 46 walihukumiwa kunyongwa kwa sababu ya kuhusika na vitendo vya kigaidi na vya kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment