Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Mkazi, Angelina Mabula (pichani) ameiagiza kampuni ya Watumishi Housing (WHC) kuzishirikisha mamlaka zingine ziwe sehemu ya mpango wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma nchini.
Alizitaja taasisi zinazopaswa kushirikishwa ni mamlaka za serikali za mitaa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Angelina alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Makao Makuu ya WHC ili kujua mradi wa ujenzi wa nyumba umefikia kiwango gani.
Alisema kama taasisi hiyo itashirikiana na mamlaka za serikali za mitaa, ambazo ndizo wenye watumishi wengi, itakuwa rahisi kufikia malengo kwa watumishi wengi kupata huduma bora ya nyumba.
Aliongeza kuwa watumishi wengi walioko kwenye halmashauri wana uhitaji mkubwa wa kupata miundombinu bora vijijini, hivyo uboreshaji huo utasaidia kujituma na kufanyakazi kwa weledi.“Nahitaji mradi huo ujikite zaidi vijijini kwa kushirikiana na halmashauri ambao ndiyo wenye watumishi, wakiwamo walimu ambao wana uhitaji wa makazi na mradi huo utakuwa ukombozi kwao,” alisema.
Alisema watumishi wengi hukataa kwenda maeneo ambayo hayana miundobinu, hivyo kama mradi huo wa nyumba utakamilika ukiwa na miundombinu ya barabara, maji na umeme itakuwa kivutio kwa watumishi kuishi katika maeneo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Dk. Fred Msemwa, alisema watumishi 150 kwa miaka 50 wamenufaika na mfuko wa serikali ulioko chini ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Mkazi .
Alisema kwa kasi hiyo ya serikali, haitakuwa rahisi kuwafikia watumishi wa umma kwa lengo la kila mmoja kumiliki nyumba kwa kulipa kidogo kidogo.
Msemwa alisema taasisi iliamua kuanzisha mradi huo wa nyumba baada ya kufanya utafiti kuhusu watumishi wanaokopa fedha benki wanazitumia kwa kufanyia kitu gani.
Alisema asilimia 44 ya watumishi wanaokopo pesa benki hupenda kujenga nyumba, hivyo WHC ikaamua kuanzisha mradi huo.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Mkazi, Angelina Mabula (pichani) ameiagiza kampuni ya Watumishi Housing (WHC) kuzishirikisha mamlaka zingine ziwe sehemu ya mpango wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma nchini.
Alizitaja taasisi zinazopaswa kushirikishwa ni mamlaka za serikali za mitaa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Angelina alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Makao Makuu ya WHC ili kujua mradi wa ujenzi wa nyumba umefikia kiwango gani.
Alisema kama taasisi hiyo itashirikiana na mamlaka za serikali za mitaa, ambazo ndizo wenye watumishi wengi, itakuwa rahisi kufikia malengo kwa watumishi wengi kupata huduma bora ya nyumba.
Aliongeza kuwa watumishi wengi walioko kwenye halmashauri wana uhitaji mkubwa wa kupata miundombinu bora vijijini, hivyo uboreshaji huo utasaidia kujituma na kufanyakazi kwa weledi.
“Nahitaji mradi huo ujikite zaidi vijijini kwa kushirikiana na halmashauri ambao ndiyo wenye watumishi, wakiwamo walimu ambao wana uhitaji wa makazi na mradi huo utakuwa ukombozi kwao,” alisema.
Alisema watumishi wengi hukataa kwenda maeneo ambayo hayana miundobinu, hivyo kama mradi huo wa nyumba utakamilika ukiwa na miundombinu ya barabara, maji na umeme itakuwa kivutio kwa watumishi kuishi katika maeneo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Dk. Fred Msemwa, alisema watumishi 150 kwa miaka 50 wamenufaika na mfuko wa serikali ulioko chini ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Mkazi .
Alisema kwa kasi hiyo ya serikali, haitakuwa rahisi kuwafikia watumishi wa umma kwa lengo la kila mmoja kumiliki nyumba kwa kulipa kidogo kidogo.
Msemwa alisema taasisi iliamua kuanzisha mradi huo wa nyumba baada ya kufanya utafiti kuhusu watumishi wanaokopa fedha benki wanazitumia kwa kufanyia kitu gani.
Alisema asilimia 44 ya watumishi wanaokopo pesa benki hupenda kujenga nyumba, hivyo WHC ikaamua kuanzisha mradi huo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment