Pichani ni Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya Kibinadamu na Mratibu wa Misaada ya dharua ambaye hivi karibuni amehadharisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zinauwezekano mkubwa kwa kukumbwa na mafuriko yatakayotokana na El-Nino
Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi kadhaa ambazo zinauwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko yatakayosababishwa na El-Nino.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya Ki-binadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Bw Stephen O’Brien, kipindi ambacho Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya El-Nino ni kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu wa 2016.
Nchi nyingine ambazo zinauwezekano wa kukumbwa na mafuriko makubwa pamoja na Tanzania ni Madagascar, Malawi na Msumbiji.
Taarifa ya Bw. O’Brien kuhusu madhara ya El-Nino na namna gani Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia hiyo iliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nakala yake kutumwa kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, pamoja na kutoa tahadhri hiyo, amewasihi nchi ambazo zinatarajiwa kukubwa na maafa ya El-Nino kujiandaa ipasavyo.Maandalizi hayo ni pamoja utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi watarajiwa wa athari za El- Nino .
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, kwa upande wa Afrika ya Mashariki, nchi kadhaa hususan ukanda kwa magharibi zimekubwa na uhaba mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa chakula. Nchi hizo ni Ethiopia Sudan, Djibouti na Eritrea, ili hali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka.
“ Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania, Msumbiji, Madagascar na Malawi zinauwezekano mkubwa kwa kukubwa na mafuriko ya El- Nino” . anatahadharisha O’Brien
Kwa mujibu wa Bw. Stephen O’Brien hichi hizo zitahitaji pamoja na mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia ya kile kinachotabiliwa kwamba kinauwezekano mkubwa wa kutokea.
Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo zinakumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na upatikanaji wa chakula ni Angola, Botswana, Malawi, Namibia, Afrika ya Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Nchi hizi zimekubwa na uhaba mkubwa wa mvua kiasi kwamba na kwa mujibu mwa Bw. Stephen O’Brien zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ambapo watu zaidi ya milioni 28 katika mataifa hivyo watakabiliwa na uhaba wa chakula
Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwisha kutolewa na nchi wahisani katika kukabiliana na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino , Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anasema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi cha dola 360 milioni kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na madhara yatakayotokana na El-Nino ukiwamo usalama wa chakula.
Pamoja na michango hiyo, Bw. O’Brien anasema haitoshi kutokana na ukweli kwamba maafa yatakayotokana na madhira ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi
Mbali ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi ulimwenguni ambazo zinatakumbwa na ama zimeshakubwa na balaa la El-Nino ni pamoja na Nchi ambao zimo katika Bara la Latini ya Amerika, na nchi za eneo la Pacific ambazo nyingi ni visiwa.
Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa ( World Meteorogical Organization) litanatarajiwa katika mwezi February kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo wa El-Nino.
No comments :
Post a Comment