Waswahili wanasema, kiburi si maungwana,
Kiburi si kitu chema, kisha hakileti mana,
Humpa mtu killema, cha mwendo wa kujiona,
Dharau si maungwana
Kiumbe acha kiburi, huko ni kujisahau,
Ishi na watu vizuri, usiwe mwenye dharau,
Onyesha tabia nzuri, hiyo ndiyo zambarau,
Dharau si maungwana.
Mpanda ngazi hushuka, daima juu hashangai,
Maisha hubadilika, ajuaye hashangai,
Usije weka tabaka, hali bado uko hai,
Dharau si Maungwana.
Kwa hayo hapa tamati, nimefika mwishoni,
Usomjua kwa dhati, hilo angalia sana,
Hutopata sirati, iendayo kwa rabana,
Dharau si maungwana.
Mwisho
/ Mwananchi.
No comments :
Post a Comment