Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 26, 2016

Vijana ACT-Wazalendo washtukia ruzuku ya utekelezaji elimu bure.

ACT-Wazalendo
Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa  Dar es Salaam, imesema imestushwa na kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa na serikali kwa ajili ya kutekeleza mpango wa elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne. 
 
Taarifa ya Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana ilisema kiasi hicho cha fedha kilichotengwa ni ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji muhimu ya upatikanaji wa elimu bora nchini.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kutekeleza mpango huo, 
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa ruzuku ya Sh.  25,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari na Sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka.
 
"Fedha hizi za ruzuku ni sawa na wastani wa Shilingi 68 kwa mwanafunzi mmoja wa sekondari kwa siku na Shilingi 27 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa siku," ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo. Kwa msingi huo, Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo imeitaka serikali iongeze kiasi hicho cha ruzuku ili kikidhi dhana ya elimu bure na mahitaji ya shule kufikia Sh. 40,000 kwa kila mwanafunzi wa  sekondari kwa mwaka sawa na wastani wa Sh. 109 kwa siku na Sh. 25,000 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka sawa na wastani wa Sh. 68 kwa siku. 
 
Aidha, wameonya kwamba fedha hizo zisitumike kwa matumizi mengine yoyote ya serikali nje ya upatikanaji wa elimu katika eneo husika. 
 
Vile vile wameshauri kuwa fedha hizo zitumwe moja kwa moja kwenye akaunti za kila shule na halmashauri zihakikishe kuwa hakuna akaunti hewa.
 
"Pia tunaiomba serikali itoe mchanganuo wa matumizi ya  fedha hizi ili kuondoa mgogoro kati ya uongozi ya shule na wazazi," imesema taarifa hiyo. 
 
 Vile vile Ngome ya vijana ACT-Wazalendo mkoani Dar es Salaam imeziomba kamati za shule na wazazi kufuatilia kwa karibu fedha hizo za ruzuku na matumizi yake kwenye shule husika. 
 
Na katika hatua nyingine, Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo mkoani Dar es Salaam imeitaka serikali kuzingatia utu wakati wa utekelezaji wa sheria kwenye suala la bomoabomoa. 
 
"Kwa kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha watu wake wanakuwa katika mazingira salama, tunaitaka iwasaidie waathirika wa bomoa bomoa hiyo hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kwa kuwapatia maeneo ya kujisitiri kwa wakati huu huku mpango endelevu wa kuhakikisha madhara kama hayo hayajirudii ukiwa unafanyiwa kazi," ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Ngome Vijana ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Karama Kaila.
 
Iliongeza: "Tunaitaka serikali katika kutekeleza sheria yake hiyo ya kuwaondoa waliojenga mabondeni, ihakikishe inawawajibisha wote waliozembea katika majukumu yao na kuwafanya wananchi kujenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa."
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment