Tangu aingie madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Magufuli amekuwa akikacha safari za nje kuhudhuria mikutano na badala yake amekuwa akiwatuma viongozi wa kiserikali kumwakilisha.
Moja ya safari ambazo Rais Dk. Magufuli hakwenda ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM), uliofanyika visiwa vya Malta, Novemba 27, mwaka jana.
Katika mkutano huo, Rais alimtuma aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe, kumwakilisha akiwa pamoja na maofisa wengine watatu.
Pia Novemba 29, mwaka jana, Rais Magufuli alitakiwa kuwapo Paris, Ufaransa, katika mkutano wa kimataifa wa 21 kujadili mabadiliko ya tabianchi duniani (COP21), ambao takriban wakuu wa nchi 150 kutoka nchi 195 walishiriki, wakiwamo marais Barack Obama wa Marekani na Xi Jinping wa China.
Desemba 5, 2015, Rais Magufuli pia hakwenda Johannesburg, Afrika Kusini, ambako kulikuwa na mkutano wa tano wa wakuu wa nchi za Afrika na Rais wa China, Xi Jinping, kupitia Jukwaa la Nchi za Afrika na China (FOCAC).
Desemba 5, 2015, Rais Magufuli pia hakwenda Johannesburg, Afrika Kusini, ambako kulikuwa na mkutano wa tano wa wakuu wa nchi za Afrika na Rais wa China, Xi Jinping, kupitia Jukwaa la Nchi za Afrika na China (FOCAC).
Katika mkutano huo, Rais Magufuli aliwakilishwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Kadhalika, Januari 31, mwaka huu, pia alimtuma Samia kumwakilisha katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika, uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia ambao ulikuwa unajadili masuala ya usalama barani Afrika.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment