Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, akiwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (kushoto) alipotembelea machinjio ya Ukonga, Dar es Salaam juzi usiku. Kushoto kwa waziri ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Said Kumbilamoto. Picha na Anthony Siame
Kutokana na hali hiyo, Nchemba aliamuru mkuu wa Mnada wa Pugu aliyefahamika kwa jina moja la Samwel akamatwe na wasaidizi wake na kupelekwa mahakamani.
“Mkuu wa Mnada wa Pugu ambaye siku si nyingi aliambiwa na Serikali na kupewa jukumu hili, leo amerudia tena kufanya haya, lakini na watumishi wote waliotajwa kwenye ubadhirifu huo nawasimamisha kazi kuanzia sasa. Pia kuanzia usiku huu nimeagiza vyombo vya dola kuwakamata na wafikishwe mahakamani, hatua nyingine za kiofisi zinaanza kutekelezwa leo,” alisema.
Januari 2, mwaka huu waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika mnada huo na kusitisha utozaji wa ushuru, badala yake aliagiza makusanyo ya fedha yafanyike Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Kutokana na mabadiliko hayo, Waziri Mwigulu alisema mnada wa Pugu utakuwa unatumika kutoa vibali vya mifugo ili kudhibiti ubora wa ile inayopaswa kuchinjwa.
No comments :
Post a Comment