Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 12, 2016

Rais Dk. Magufuli ameanza vizuri, atekeleze ahadi zote

NA EDITOR

12th February 2016.

Katuni.
Rais Dk. John Magufuli, leo ametimiza siku 100 madarakani tangu alipoapishwa kushika nafasi hiyo Novemba 5, mwaka jana.
 
Katika siku hizo amejielekeza katika kushughulikia mambo kadhaa yenye maslahi kwa taifa, ikiwamo kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, kuweka nidhamu katika matumizi na kupambana na ufisadi.
 
Pia, Rais Magufuli ameanza kwa kuelekeza fedha zinazopatikana katika taasisi kadhaa za umma ambazo zilikuwa zinakabiliwa na hali ngumu ya kifedha pamoja na kuboresha huduma muhimu za jamii.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili ilinunuliwa vitanda 300 na magodoro yake kutokana na Sh. milioni 200 ambazo alizuia zisitumike katika sherehe ya wabunge kupongezana baada ya kuzinduliwa kwa Bunge la 11, Novemba 20, mwaka jana.
 
Kiasi kingine Sh. bilioni nne ambazo zingetumika katika maadhimisho ya siku ya  Uhuru wa Tannzania Bara zilipelekwa kwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kujenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es Salaam.Rais Magufuli pia ameipatia Mahakama ya Tanzania Sh. bilioni 12.3 kwa ajili ya kumaliza kesi mbalimbali pamoja na maendeleo ya mahakama kwa ujumla, ikiwamo kujenga na kukarabati majengo ya mhimili huo. Aidha, katika awamu ya kwanza, Sh. bilioni 18.8 zilipelekwa kutoa elimu bure katika shule za sekondari na msingi. 
 
Katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, serikali imechukua hatua ya kuwasaka wafanyabiashara ambao walipitisha makontena bandarini bila kuyalipia kodi na kuwabana walipe fedha hizo, huku nidhamu ikisimamiwa na kuzuia safari za nje za watumishi wa serikali ambazo hazina tija. Kadhalika, semina, mikutano na makongamano vimedhititiwa sambamba na kutotumia hoteli kufanyia mikutano. Yote hayo yakiwa na lengo la kubana matumizi ya serikali.
 
Kwa kuangalia mambo aliyoanza kuyatekeleza ndani ya siku 100, tunasema kuwa Rais Magufuli ameanza vizuri, ingawa anakabiliwa na na changamoto nyingi na kubwa. Changamoto zinahusu ukamilishaji wa mambo aliyoyaanza na yale ambayo hajayaanza.
 
Kwa mfano, aliahidi kwamba serikali ingeanzisha mahakama ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, lakini sasa inaelezwa kuwa mahakama hiyo itaanza ndani ya mwaka mmoja. Rais Magufuli vilevile, aliahidi kwamba atatoa Sh. milioni 50 kwa kila kijiji nchini, ahadi ambayo hajaanza kuitekeleza hadi sasa.
 
Licha ya kuahidi kuboresha huduma za afya katika hospitali nchini, lakini ameonekana kujikita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tu kwa kuipatia vitanda na magodoro pamoja na mashine za T-scan na MRI,  wakati hospitali nyingi za serikali nchi nzima zinakabiliwa na matatizo mengi.
 
Sekta ya elimu ambayo ameanza kutekeleza ahadi yake ya elimu bure, inakabiliwa na changamoto nyingi. Shule zinakabiliwa na hali mbaya ikiwamo wanafunzi kusomea chini ya miti kwa kukosa madarasa. Hili ni eneo mabalo atatakiwa kuliangalia kwa umakini kwa kuelekeza fedha zaidi.
 
Kinachotakiwa ni kwamba elimu bure iwe elimu bora na kwa msingi huo shule hizo zitapaswa kuboreshwa sambamba na kuongeza idadi ya walimu na mahitaji mengine ikiwamo serikali kutoa ruzuku ya chakula kwa shule za kutwa.
 
Kwa kuwa ajenda kuu ya serikali ya awamu ya tano ni Tanzania kuwa nchi ya viwanda, shule zetu hazinabudi kuboreshwa ili zikidhi viwango, kwani itakuwa ndoto kuwa na wanasayansi na wahandisi wa kufanya kazi katika viwanda tunavyodhamiria kuvianzisha ambao wanasomea chini ya miti. Tunampongeza sana, lakini tunamkumbusha atekelezea ahadi zake zote.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment