Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 13, 2016

ZEC: Ngoma Inogile


Kama ilivyopokewa:

“Habari zinaarifu kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imegoma kuondoa picha za wagombea Urais, Udiwani na Uwakilishi kutoka vyama vilivyotangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio, ikiwemo jina na picha Maalim Seif Sharif Hamad.

Hilo lilifahamika jana mjini Unguja, baada ya kigogo mmoja wa ZEC ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, kusema kuwa sheria hazimruhusu mgombea yeyote kujitoa mwenyewe kwa utashi wake binafsi.

Kiongozi huyo alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3…6 cha sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, mgombea hawezi kujiondoa kwa utashi wake baada ya tume kukamilisha kazi ya uteuzi ambayo ilifanyika kabla ya Oktoba 25 mwaka jana.

“Ieleweke kwamba mgombea urais anaweza kujiondoa katika kinyang’anyiro kwa kuwasilisha taarifa za maandishi yeye mwenyewe Ofisi za ZEC, kabla ya saa 10 jioni ya siku ya uteuzi,” alisema ofisa huyo akinukuu kifungu cha katiba.


Mohammed Ghassani – ‘facebook page’

No comments :

Post a Comment