Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 13, 2016

Zuma afuata nyayo za Magufuli

Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma     
Pretoria, Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma juzi usiku alipata wakati mgumu kuelezea vipaumbele vyake bungeni baada ya hotuba yake kukatizwa mara kwa mara na wabunge wa upinzani na kufanikiwa kutaja mikakati yenye kubana matumizi.
Awali, kabla ya hotuba hiyo kulijitokeza mvutano wa wazi kati ya Spika, Baleka Mbete na wafuasi wa upinzani wengi wao kutoka chama cha Ecoomic Freedom Fighters (EFF) waliokuwa wakiongozwa na Julius Malema.
Wakati wote wabunge hao walisimama na kuomba mwongozo katika kile kilichoonekana kama mkakati wa wazi wa kuvuruga hotuba ya Rais Zuma.
Baada ya mvutano wa dakika kadhaa, Spika Mbete alionekana kushindwa kuendelea kuvumilia na ndipo alipoamuru kiongozi wa EFF, Malema kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge.
Baada ya fujo hizo, Rais Zuma aliendelea kuhutubia, lakini wabunge wa upinzani waliobaki kurudia tena kumkatiza.
Baada fujo hizo baadaye kulitokea utulivu na kutoa mwanya kwa Zuma kuendelea na hotuba yake. Katika hotuba hiyo, Rais huyo alisema Serikali yake imekuwa ikibana matumizi, lakini hatua zaidi zinahitajika.
Alisema kuanzia sasa Serikali yake itachukua hatua muhimu ya kuendelea kubana matumizi ikiwamo kupunguza safari za nje.
Alisema watumishi wanaotaka kusafiri nje ya nchi watalazimika kupata ruhusu maalumu kutoka ofisi yake.
Pia, aligusia kuhusu kupunguza gharama za mikutano ya mara kwa mara akisema ya namna hiyo itaanza kuangaliwa na ile itakayobainika kutokuwa na tija gharama zake zitaondolewa.
Hatua ya Rais Zuma inatajwa kufanana na ile inayochukuliwa na Rais John Magufuli ambaye amekuwa akihimiza sera ya kubana matumizi huku akiwataka watumishi wa umma kuwajibika. Rais Magufuli amepiga marufuku safari za nje, sherehe na shughuio nyingine za Serikali ili kuokoa mamilioni ya fedha na kutumika kutatua kero nyingine katika jamii, ikiwamo katika sekta za afya na elimu. Tangu aingie madarakani mwaka jana, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa watendaji kadhaa.    

No comments :

Post a Comment