Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 16, 2016

Wakosoa utekelezaji wa Bajeti

Profesa Honest Ngowi 
By Elias Msuya, mwananchi 
Dar es Salaam. Baadhi ya Wataalamu wa uchumi nchini wamekosoa utekelezaji wa Bajeti ya 2015/2016 na kuonya kuwa Bajeti ya mwaka ujao haitakuwa na jipya.
Vipaumbele vya Bajeti hiyo vilikuwa kuendeleza Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao unajumuisha maeneo sita ya kitaifa ya kilimo, elimu, maji, utafutaji wa rasilimali fedha, nishati, uchukuzi na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wachumi hao pia wameonya hatua ya Rais John Magufuli kubana matumizi kuwa itazidi kuharibu uchumi badala ya kuujenga.
Profesa wa Uchumi, Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema Bajeti ya mwaka 2015/2016 kama zilivyokuwa nyingine zilizopita, haikutekelezeka kikamilifu kwa sababu ya matumizi mabaya.
“Kwa ujumla bajeti zetu hazitekelezeki kwa sababu ya kukosa nidhamu ya matumizi. Fedha zinaweza kutolewa hata kama ni kidogo lakini zinatumika kwenye chai na ununuzi wa vitu visivyo na tija kwa Taifa,” alisema.
Hata hivyo, alisema hatua za Rais Magufuli kubana matumizi zinaweza kufanikisha bajeti kama fedha hizo zitapelekwa maeneo husika kwa wakati “...tunaweza kutekeleza bajeti kwa kiasi kikubwa hata kama haitafikia asilimia 100, inaweza kufikia asilimia 75.”
Profesa Damian Gabagambi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro alisema Bajeti ya 2015/2016 haina tofauti na za nyuma ambazo alisema ni za takwimu bila uhalisia.
Kuhusu utekelezaji wa BRN alisema kilichopangwa na kinachofanyika ni vitu viwili tofauti kabisa: “Sioni tofauti ya utekelezaji wa bajeti wa miaka mingine na hii inayoishia hasa kwa kuangalia kisekta. Nilishiriki kuandaa BRN, najua tulichopanga, najua tulipanga kupata fedha wapi na tutafika wapi.
Kinachofanyika siyo kile tulichopanga. Wamebaki wataalamu tu kutoa takwimu lakini utekelezaji haupo. Kero za wakulima ziko palepale, hawana masoko, hawana pembejeo, hawaruhusiwi kuuza mazao yao nje.”
Alionya hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kubana matumizi ya Serikali kuwa zitadidimiza zaidi uchumi badala ya kuuinua.
“Kubana matumizi ya Serikali ni sawa kama kutafanyika kimkakati, vinginevyo ndiyo uchumi utaanguka kabisa. Kwa sababu ni lazima ujue uchumi wa dunia uko wapi... tusipokuwa makini uchumi wetu utaanguka tu. Kwa mfano, Rais Magufuli amesema mikutano yote ya taasisi za Serikali ifanyikie kwenye majengo ya taasisi hizo, lakini ajue hata kwenye zile hoteli wanalipa kodi ya Serikali na wanapata fedha za kulipa wafanyakazi ili waishi. Kwa hiyo hoteli zitafungwa wafanyakazi watakwenda wapi?,” alihoji.
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe, alisema Bajeti ya mwaka 2015/2016 haikutekelezeka ipasavyo kwa sababu ya kutotolewa kwa fedha zinazoidhinishwa na Bunge kikamilifu.     

No comments :

Post a Comment