Aliyasema hayo wakati akikabidhiwa wizara hiyo na mtangulizi wake, iyo Ramadhani Abdallah Shaaban, ambaye ni mmoja wa mawaziri wa zamani walioachwa na Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika awamu yap ili ya serikali yake.
Salama alisema lazima kila mfanyakazi kuzingatia muda wa kufika na kutoka kazini na kuhakikisha wanachapa kazi ili kuwatumikia Wazanzibari.Alisema hatakuwa na mzaha katika kazi na yule ambaye hayuko tayari kufanya kazi, ni bora apumzike ili apishe nafasi kwa wanaotaka kufanya kazi.
Aidha, aliitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa) kuhakikisha inatoa huduma bora ya maji safi na salama kutokana na kuibuka kwa kipindupindu. Alisema asilimia kubwa ya kipindupindu inasababishwa na maji machafu wanayopata wananchi.
Naye Shaaban, alisema anajisikia furaha kuona anamkabidhi wizara hiyo mwanamke lakini pia kutoka CCM.
Alisema licha ya mambo mbalimbali ya kimaendeleo aliyoyafanya akiwa katika wizara hiyo, bado kuna changamoto nyingi za kimaendeleo, zikiwamo makaazi, maji na nishati ya umeme.
Alimwomba waziri huyo mpya kujikita zaidi katika mambo hayo kwa kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na bila vitu hivyo, maendeleo ya haraka hayawezi kupatikana.
Alimtaka waziri huyo mpya kuendeleza hatua ambazo alishazianza katika kujenga uchumi hasa katika uchimbaji wa mafuta na gesi.
No comments :
Post a Comment