Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, June 20, 2016

Kashfa michoro uwanja wa ndege Zanzibar

Picha: Ni jengo linalotumika sasa kwa shughuli za uwanja wa ndege (Karume Airport), Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imepata hasara ya dola za kimarekeni milioni 58.3 baada ya michoro (ramani) ya ujenzi wa jengo la abiria linaloendelea kujengwa kukosewa, imefahamika mjini Zanzibar, jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) imesema gharama za mradi huo zimeongezeka kutoka dola za kimarekani milioni 70 .4 mwaka 2009 mpaka dola milioni 128.7 kutokana na kukosewa kwa michero ya jengo hilo.
Akiwasilisha taarifa ya kamati Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Suleiman Sarahan alisema kuwa mradi huo umebainika kuwa na matatizo ya michoro ya ramani ya ujenzi na kusababisha gharama za marekebisho mara mbili tangu kuanza kwa mradi huo.
“Mheshimiwa Spika kamati yangu imegundua kulikuwa na mapungufu katika mchoro wa awali ikiwemo maegesho ya ndege kuwa karibu mno na jengo la abiria, pamoja na njia ya kurukia ndege kuwa juu kuliko jengo lenyewe.”alisema Sarahan.
Alisema kuwa matatizo yaliyojitokeza ya michoro yamesababisha marekebisho ya gharama za ujenzi kufanyika mara mbili ili kuokoa mradi huo lakini mpaka sasa umekwama na hakuna watu waliofikishwa katika vyombo vya sheria.
Sarahan alisema matatizo mengine yaliyobainika ni kwamba, jengo limejengwa bila kuwepo njia za kupitisha maji ya mvua jambo ambalo linaweza kusababisha hasara ya mali na vifaa hapo baadaye na kuhatarisha usalama wa uwanja wakati wa mvua.
“Mheshimiwa Spika tatizo hili linaweza kuleta uharibifu mkubwa wa mali na vifaa hapo baadae wakati wa mvua kama hazitachukuliwa hatua za dharura ikiwemo kujenga mitaro ya kupitishia maji ya mvua.”alisema Sarahan huku baadhi ya wajumbe wakitikisa vichwa.
Alisema kuwa wakati umefika kwa serikali ya SMZ kujitathimini, kujiridhisha na kuwa makini wakati wa kuingia mikataba ya miradi mikubwa ya maendeleo ili kuepusha hasara zinazojitokeza katika miradi ya ujenzi wa miundo mbinu.
Alisema kuwa katika mradi huo tayari serikali imelazimika kufanya marekebisho ya gharama za mradi mara mbili baada ya mara ya kwanza kuongeza dola milioni 11.8 June mwaka 2012 pamoja na dola milioni 46.5 April mwaka 2014 na kufikia jumla ya dola za kimarekani milioni 128.7 lakini mradi huo umeshuindwa kukamilika.
“Sisi wajumbe tangu ulipoanza mradi huu tulianza kutilia mashaka jinsi ya ushirikishwaji wa wadau mbali mbali, jambo ambalo lilitawaliwa na manung’uniko miongoni mwa watendaji wa serikali na hata wajumbe kuzuia bajeti kutokana na kizungunkuti cha ujenzi wa mradi huo,” alilalamika Sarahan Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake Pemba.
Hata hivyo taarifa za ndani zinasema kuwa jengo hilo linahitaji kuvunjwa na kujengwa upya au serikali itowe fedha nyingine karibu dola milioni 14 kufanya marekebisho makubwa ya ujenzi wake.
Hata hivyo, kamati hiyo imesema kuwa mradi huo umekuwa na matatizo makubwa na kusababisha hasara kwa serikali kutokana na wadau mbalimbali kutengwa na Wizara ya Fedha Zanzibar, wakiwemo wahusika wakuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Zanzibar (ZAAA), wakati wa matayarisho ya ujenzi wa mradi huo.
/Nipashe

4 comments :

  1. Business as usual, au tunasema " RISKI HAIWANWI" wakati tutakuwa wazembe kupita kiasi !!! Maana njia moja ya kuondoa msongamano wa makontena matupu ni kuweka bei kubwa, jambo ambalo litawasababishia upungufu wa mapato kwa maana meli zitaacha cotena tupu aidha dsm au msa, njia ya pili ni kutumia ile " bandari kavu" SAATENI, na meli zikija kupakia contena zao zipakiwe usiku ili kiepusha msongamano wa ile njia kuu ya mjini/kaskazini .....
    2. Huu uwanja wa ndege utasema tunajenga piramid za Misri, haumaliziki na gharama zinaongezeka, watu wanafuja fedha wa wananchi na Hamna anowauliza wala kuwajibishwa madam ni wa kile chama chetu cha nanihii, nahisi nao utashinda na itakuwa kama ule mradi wa e-government wa smz , walipokabidhiwa watakuta sehemu nyingi hazifanyi kazi , wajenzi walipoulizwa wakasema tukipewa pesa tutarekebisha " mara hii haitukuwa hivyo " fedha za wanyonge hizo jamani ......au ndo mtu akiwa mkubwa smz hawajibishwi madam sio wa chama kile ?

    ReplyDelete
  2. I wanted to thank you for this excellent read!! I definitely loved every little bit of it. I have you bookmarked your site to check out the new stuff you post. Zanzibar taxi

    ReplyDelete
  3. I can’t believe focusing long enough to research; much less write this kind of article. You’ve outdone yourself with this material without a doubt. It is one of the greatest contents. Zanzibar taxi

    ReplyDelete
  4. Zanzibar car rental Thanks for a very interesting blog. What else may I get that kind of info written in such a perfect approach? I’ve a undertaking that I am simply now operating on, and I have been at the look out for such info.

    ReplyDelete