Mji wa Les Cayes, Haiti unavyoonekana kwenye picha baada ya kukumbwa na kimbunga Matthew siku ya Alhamisi Oktoba 6, 2016.
Mwanamke wa mji wa Baracoa nchini Cuba akiangua kilio baada ya nyumba yake kubomolewa na kimbunga Matthew.
Watu wakijaribu kuvuka mto La Digue siku ya Jumatato Octoba 5, 2016 nchini Haiti ambapo kimbunga cha Matthew kimesababisha watu 269 kupoteza maisha.
Wanajumuiya ya Carbonera mji wa Guantanamo nchini Cuba wakirejea kwenye makazi yao siku ya Jumatano Oktoba 5, 2016 baada ya kimbunga Matthew kuleta madhara kwenye mji huo.
Watu wakiwa wamesimama ufukweni kaunti ya Broward, Florida wakati upepo wa kimbunga Matthewulipokua ukivuma kwa spidi ya maili 120 kwa saa siku ya Alhamisi Octoba 6, 2016 siku ambayo pwani ya Florida ilikumbwa na kimbunga hicho ambacho kimekua tishio kwa watu na mali zao
Wakazi wa mji wa Les Cayes, Haiti wakikarabati nyumba zao baada ya kimbunga Matthew kuleta madhara makubwa ikiwemo watu 269 kupoteza maisha.
Hii ni siku ya Jumatano Oktoba 5, 2016 watu wakiwa kwenye foleni kubwa ya magari barabara ya I 26 wakijaribu kuhama mji wa Columbia, uliopo jimbo la Corolina ya Kusini kujinusuru na kimbunga Matthew ambacho awali kilitangazwa kupita maeneo hayo ya mji huo.
Afisa wa Polisi akifanya doria ufukweni mwa kisiwa cha Singer kilichopo Florida.
Mvua za kwanza za kimbunga Matthew na upepo mkali na wingu kubwa zikiwa zimetanda katika mji wa Orlando, Florida siku ya Alhamisi Octoba 6, 2016.
Gari la doria likiangalia usalama kwenye ufukwe wa mji wa Jacksonville, Florida.
Wananchi Miami Florida wakijiandaa kwa kuweka mbao kwenye madirisha ya nyumba zao siku ya Alhamisi Octoba 6, 2016.
Watu wakiwa wamebeba jeneza la mpendwa wao wakijaribu kuvuka mto La Digue kutokana na daraja la Petitt-Goave kuvunjika kutokana na kimbunga Matthew.
Hapa ni mji wa Baracoa nchini Cuba watu wakiumbatiana kujifariji baada ya kimbunga Matthew kuleta madhara kwenye mji huo.
/CNN.
No comments :
Post a Comment