Waziri asiekuwa na Wizara Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP Said Soud Said akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kuwataka Wazanzibari kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi,katika ukumbi wa Jumba la Utamaduni Rahaleo Zanzibar.
Waziri asiekuwa na Wizara Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFPSaid Soud Said akifafanua jambo alipofanya mazungumzo na Waandishi wa Habari kuhusiana na kuwataka Wazanzibari kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi,katika ukumbi wa Jumba la Utamaduni Rahaleo Zanzibar.kulia ni Mkuu wa Habari Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri asiekuwa na Wizara Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP Said Soud Said alipofanya mazungumzo nao kuhusiana na kuwataka Wazanzibari kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi,katika ukumbi wa Jumba la Utamaduni Rahaleo Zanzibar.
Muandishi wa Habari kutoka Hits FM Jazaa Kombo akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri asiekuwa na Wizara Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP Said Soud Said kuhusiana na kuwataka Wazanzibari kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi,katika ukumbi wa Jumba la Utamaduni Rahaleo Zanzibar.
Muandishi wa Star Tv Abdalla Pandu akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri asiekuwa na Wizara Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP Said Soud Said kuhusiana na kuwataka Wazanzibari kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi,katika ukumbi wa Jumba la Utamaduni Rahaleo Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Na Mwanaisha Mohammed-Maelezo
Wazanzibari wametakiwa kujikusanya na kuanzisha makampuni makubwa ya kuwekeza badala ya kusubiri wawekezaji kutoka nje ili kusaidia jamii na kuharakisha maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika studio ya zamani ya utangazaji Rahale, Mwenyekiyi wa Chama Cha Wakulima (AFP) Said Soud amesema wazanzibari wanayo nafasi nzuri ya kuwekeza hasa katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu, kilimo na ufugaji pamoja na michezo.
Saidi Soud ambae pia ni Waziri asiekuwa na Wizara maalum katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema iwapo wananchi watajikusanya na kutafuta wafadhili kwa ajili ya kuwekeza wataweza kuisaidia nchi kwa kuwapatia vijana ajira badala ya vijana wengi kusubiri ajira za serikali baada ya kumaliza masomo.
“Wawekezaji wazalendo wananafasi kubwa katika kuhudumia jamii bila kusubiri wawekezaji kutoka nje kuwekeza vitega uchumi vyao, ”alisisitiza Mwenyekiti wa chama cha AFP.
Alisema ni jambo zuri kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje kwa vile wanakuja na teknolojia ya kisasa lakini jambo zuri watakapofika wakute wazalendo wenyewe wanaendelea kuwekeza.
Amewashauri wananchi kuwa wabunifu na kuachana na uvvivu wa kufikiri ili kupiga hatua ya haraka kuleta maendeleo.
“Wazanzibar acheni dhana ya kufikirishwa kuna fursa nyingi za kuwekeza ambazo zitapelekea kujikwamua na umasikini,”alisema Said Soud.
Aliishauri jamii kujituma na kutumia rasilimali na fursa nyingi zilizopo huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira mazuri ya wananachi kuendeleza shughuli zao za maisha na kupunguza umasikini.
Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, amesema ni nzuri na amewataka wananchi kuvipuuza vikundi na wanasiasa wanaozungumzia kufanyika uchaguzi mwengine kabla ya mwaka 2020.
Amewataka wananchi kuelekeza nguvu zao katika kufanyakazi badala ya kusikiliza maneno ambayo hayana tija kwao na hayasaidii kuharakisha maendeleo yao.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments :
Post a Comment