Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mahafali ya pili yaliofanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku mmoja wa wahitimu kati ya wahitimu 133 waliohitimu leo na kutunukiwa Shahada na Stashahada.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sudan Mhe.Mahgoub Ahmed Sharfi , ambapo mabalozi mbali mbali walihudhuria.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Mabalozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa Wizara, Idara na taasisi za Serikali zina matumizi madogo ya takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini hali ambayo inachangia kurudisha nyuma shughuli za upangaji wa maendeleo za wananchi.Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo trh 19-Nov-2016 katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, Idara na taasisi za Serikali kuimarisha matumizi ya takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga na kuweka mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika uimarishe ushirikiano na Wakuu wa Takwimu wa Afrika kwa kuhakikisha watakwimu wanaoingia katika soko la ajira wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya kisheria na kanuni zake katika ukokotoaji wa takwimu zinazokubalika kitaifa na kimataifa ambazo zitawezesha Afrika kupanga maendeleo ya wananchi kwa ufanisi mkubwa.
Amewahimiza wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pindi watakapoanza kufanya kazi zao wafanye kazi kwa ufanisi na kwa umakini wa hali ya juu ili kutimiza azma ya kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 katika bara la Afrika.
“Wito wangu kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaimarisha vitengo vya takwimu kwa kuwaruhusu maofisa waliopo katika vitengo vyao vya sera na mipango wapate fursa ya kupatiwa mafunzo elekezi na ya muda mfupi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao wa kuchambua na kukokotoa takwimu rasmi”
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa hategemei kuona wahitimu walio maliza masomo yao katika ngazi mbalimbali katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wamalize soli za viatu kusaka ajira na kwamba Serikali itawawekea mazingira bora ya kupata ajira haraka.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kutumia takwimu sahihi ambazo zimetolewa na ofisi hiyo katika kupanga shughuli za maendeleo za taifa.
Katika mahafali hiyo ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewatunuku vyeti wahitimu 133 katika ngazi za Shahada ya Uzamili ya Takwimu, Shahada ya awali ya takiwmu na Stashahada ya takwimu kwa wahitimu kutoka nchi Kumi za Afrika ambazo ni Nigeria,Ghana,Sierra Leon, Ethiopia,Somalia, Uganda, Swaziland, Liberia, Rwanda na mwenyeji Tanzania.
No comments :
Post a Comment