Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar
Shirika la Ndege la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba 13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.
Shirika hilo maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote, zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.
Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244 ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo.
Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.
Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.
Safari ya kwanza itazinduliwa Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.
Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST)zitakuwa tatu kwa wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo:
Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya safari:
Namba ya ndege
|
Kuanzia
|
Siku
|
Kuondoka
|
Kuwasili
| ||
TK 567
|
14 Desemba 2016
|
Jumatatu Jumatano Jumamosi
|
Istanbul
|
20:30
|
3:20 (+1)
|
Kilimanjaro
|
TK567
|
15 Desemba 2016
|
Jumanne Alhamis Jumapili
|
Kilimanjaro
|
04:15
|
5:30
|
Zanzibar
|
TK 567
|
15 Desemba 2016
|
Jumanne, Alhamis Jumapili
|
Zanzibar
|
06:25
|
13:45
|
Istanbul
|
No comments :
Post a Comment