dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 17, 2016

WHO yasema hakuna ugonjwa wa Zika Tanzania!

Mwakilishi wa shirika Afya Duniani nchini Tanzania, Dk Grace Saguti.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa Tanzania na hakujawahi patikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.

Hayo yamesemwa leo (Jumamosi) na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.

"WHO inafanya kazi na wizara ya afya kufatilia taarifa za magonjwa unaofanyika kila siku katika maeneo yote ya afya, na taarifa huletwa wizarani kisha tunashirikishwa ili kutoa katika tovuti yetu, nachoweza kusema hatujapata taarifa za magonjwa ambazo zinazoonyesha dalili za mgonjwa yoyote mwenye zika Tanzania," amesema Dk Saguti.

Pia, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya ina mfumo maalum wa kupata taarifa za magonjwa na hakuna taarifa iliyoonyesha uwepo wa ugonjwa wa zika.

"Hakuna mgonjwa yoyote wa Zika Tanzania…narudia mara ya pili hakuna mgonjwa wa zika Tanzania," amesema Dk Kambi.

No comments :

Post a Comment