Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 31, 2017

Mualiko wa Trump wamueka malkia katika hali ngumu!

Trump na Malkia

Uamuzi wa waziri mkuu wa Uingereza Bi Theressa May wa kumualika rais Donald Trump wa Marekani umemuweka malkia katika hali ngumu, kulingana kiongozi wa zamani wa afisi ya maswala ya kigeni nchini humo.

Katika barua alioandika kwa gazeti la The Times, Lord Rickets amesema kuwa ombi hilo lilifanywa mapema mno.

Ombi la kutaka ziara hiyo ya Donald Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali limefaulu kupata zaidi ya saini milini 1.5.

Siku ya Jumatatu, maelefu ya watu nchini Uingereza waliunga maandamano dhidi ya agizo la usafiri la Donald Trump kuhusu mataifa saba ya kiislamu.Mkakati huo wa uhamiaji wenye utata ulizua mjadala bungeni.

Lord Rickets ambaye alikuwa katibu wa maswala ya kigeni kutoka mwaka 2006-10 alisema kuwa sio jambo la kawaida kwa rais wa Marekani kualikwa kwa ziara ya kitaifa katika mwaka wa kwanza wa utawala wake.

Alihoji iwapo bw Trump alistahili heshima hiyo .

''Ingekuwa vyema kusubiri na kuona ni kiongozi wa aina gani kabla ya kumshauri Malkia kumualika.Sasa Malkia amewekwa katika hali ngumu sana'',aliongezea kiongozi huyo.

No comments :

Post a Comment