BY PIUS YALULA ON FEBRUARY 26, 2017
Aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa Serikali atakayoiunda haitakuwa na waziri mzigo hata mmoja.
Amesema kuwa ataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), itakayokuwa na nguvu katika kutekeleza majukumu ya kazi yake na kuinua kipato kwa Wananchi.
Aidha, amesema kuwa katika Serikali hiyo haitakuwa na waziri mzigo hata mmoja kwa kuwa atawajibika katika majukumu yake ipasavyo na si vinginevyo.
“Sitawaangusha Wazanzibari nikikabidhiwa madaraka, kwa kuwa dhamira yangu ni kuleta mabadiliko ya maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Visiwa hivi,”amesema Maalim Seif.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akikamilisha ziara yake ya siku kumi Kisiwani Pemba na kufungua majengo ya chama hicho yakiwemo matawi na kuzindua waratibu wa chama.
Hata hivyo licha ya malalamiko ya mara kwa mara ya Maalim Seif na CUF juu ya kudhulumiwa ushindi, Rais Zanzibar Dkt. Shein amekuwa akisema chama hicho cha upinzani kisubiri Uchaguzi Mkuu utakao fanyika mwaka 2020 na kuendelea kulalamika kila kukicha.
No comments :
Post a Comment