Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, February 26, 2017

Taarifa ya Hitma ya Marehemu Abdallah Khelef Shauri Mjaka (DULLA KHELEF) Itakayofanyika Nyumbani Kwao Kibweni Zanzibar Siku ya Jumatatu 27-2-2017 Alasiri Kwa Wanaume na Wanawake!

INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUN!


Ukoo wa Shauri Mjaka na Wajukuu Wao Wanatangaza Hitma ya Ndugu yao Marehemu Abdallah Khelef Shauri Mjaka(DULLA) kilichotokea Nchini Norway wiki iliopita.

Inawatangazia Hitma Ndugu na Jamaa na Waislamu wote kuhudhuria hitma hiyo itakayofanyika nyumbani kwao Kibweni Zanzibar baada ya Sala ya Alasiri kwa Wanawake na Wanaume, kwa upande wa hitma ya wanawake itasomwa nyumbani kwao hapo kibweni na wanaume itafanyika katika msikiti wa kibweni jirani na nyumbani kwao.

Kabla ya kusomwa hitma itafuatia Sala ya kumsalia Maiti katika msikiti huo na wakati wa alasiri na kufuatiwa na hitma siku hiyohiyo. Tukiungana na Waislamu wezetu wa huko Norway wakati wakiwa katika Sala ya maiti siku hiyo ya jumatatu tarehe 27-2-2017.

Waislamu wote mnaalikwa kuhudhuria hitma hiyo na Sala ya kumsalia Maiti.

Pia Siku hiyo jumatatu 27-2-2017,mwili wa marehemu utazikwa katika makaburi ya Waislam Skonger Nchini Norway kwa saa za huko itakuwa saa 6 mchana kwa saa za Norway.

MOLA AMLAZE PEMA PEPONI MAREHEMU!

No comments :

Post a Comment