Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 18, 2017

Makonda kuchunguzwa, endapo malalamiko yakipelekwa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma!


SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema ipo tayari kuhakiki mali za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, endapo watapokea malalamiko kutoka kwa wanaomtilia shaka.

Hivi karibuni wakati akitangaza orodha ya watu wanaotuhumiwa kuuza, kuagiza na kutumia dawa za kulevya, Makonda alijikuta akiingia katika vita ya maneno na wabunge.

Msingi wa vita yenyewe ni hatua ya baadhi ya wabunge kupinga utaratibu alioutumia Makonda kuwataja kwa majina watuhumiwa hao na hata kwenda mbali zaidi wakimtuhumu na kuhoji alikopata utajiri wa ghafla.

Hatua ya kuhoji mali za Makonda ilichochewa na kauli ya Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alionekana kukerwa na ukosoaji wa wabunge hao na hivyo kuwatuhumu wawakilishi hao wa wananchi kulala bungeni na kuitikia kila kitu ndiyoooo.
Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi lililotaka kupata ufafanuzi kwa upande wa sekretarieti hiyo juu ya madai hayo ya utajiri wa Makonda na iwapo aliziorodhesha kama sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya 1995 inavyoelekeza, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa sekretarieti hiyo, Joseph Ishengoma, alisema chombo hicho kipo tayari kufanya uhakiki endapo watapokea malalamiko rasmi kutoka kwa wananchi au wabunge waliosikika hivi karibuni wakizungumzia suala hilo bungeni.

Alisema kinachotakiwa ni kufuata utaratibu ambao ni kupeleka malalamiko kwa sekretarieti hiyo kuomba kufanyika kwa uhakiki wa mali za kiongozi huyo kutokana na tuhuma walizozitoa.

Kauli hiyo ya sekretarieti imekuja ikiwa imepita takribani wiki moja sasa tangu wabunge na Makonda washambuliane kwa maneno.

Miongoni mwa wabunge walioonekana kukerwa na kauli pamoja na utaratibu alioutumia Makonda na hata kutaka naye achunguzwe ni Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, ambaye alikwenda mbali na kutaja mali zinazodaiwa kumilikiwa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akichangia taarifa za Kamati za Bunge za Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Selasini alisema Makonda amenunua jengo (apartment) lenye thamani ya shilingi milioni 600.

“Makonda amenunua apartment pale Viva Towers kwa shilingi milioni 600, Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedez Benz lenye thamani ya Dola 250 za Marekani (shilingi milioni 550) kama zawadi ya birthday,” alisema Selasini.

No comments :

Post a Comment