Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 25, 2017

STEVE NYERERE AKANUSHA WEMA KUTOLIPWA NA CCM!

Image result for STEVE NYERERE NA WAANDISHI WA HABARI


Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar Steve Nyerere amesikitika sana kwa kitendo cha mama Wema kumrekodi na kusambaza maongezi yao kwenye mitandao kwa kile alichokiita kwa nia ya kuchafulia jina.

Akiongea huku machozi yakimlenga, Steve Nyerere amesikitika na kauli alizotoa Wema Sepetu wakati akikihama chama Cha Mapinduzi kwa kusema CCM bado haijawamalizia alibaki yao ya kampeni ya mama ongea na mwanao ambayo Steve Nyerere ndiye aliyekua mwenyekiti na Wema kuwa makamu mwenyekiti.

Steve Nyerere aliongezea kuwa katika kampeni ile CCM waliwalipa wasanii wote na hakuna msanii hata moja anayeidai CCM.

Pia msanii huyo wa vichekesho aliomba radhi viongozi aliowataja kwenye maongezi yale ya yeye na mama Wema na kuwaelezea waandishi wa habari kwamba ilibidi aseme vile kwa kumridhisha mama Wema na kujaribu kutuliza mzuka kwani kulikua na fununu tayari Wema anahamia CHADEMA.
Steve Nyerere aliwaambia waandishi wa habari maungumuzo yote hasa kile alichokizungumza hakikua cha kweli kwa ilibidi atengeneze maneno ili kumridhisha mama Wema.

Katika kuijibu moja ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari kwamba wataaminije na hayo anayoyasema leo ni kuwaridhisha wao, Steve Nyerere alisema huu ndio ukweli na alitaka kuweka sawa kuhusiana na maelezo ya Wema kwamba hawakulipwa na kuongezea kwamba katika wasanii wote Wema ndiye aliyachukua hela ndefu kuliko wote.

Nasabu nyingine aliyowaita waandishi wa habari ni kutaka kuwaomba radhi viongozi aliowataja na kwamba yeye hana ugomvi wowowte na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda'

No comments :

Post a Comment