TAARIFA KWA UMMA
Tovuti ya mzalendo jumanne February 21, 2017 ilichapisha habari kuu katika ukurasa wake wa kwanza inasomeka “Htimisho la Ziara ya Rais wa Zanzibar ambae pia ni katibu mkuu wa CUF mhe. Maalim Seif katika wilaya ya wete Pemba”Taarifa hiyo iliyochapishwa katika tovuti hiyo iliyomkariri mtu anaejitambulisha kuwa ni Naibu Mkurugenzi wa habari uenezi wa JUVICUF Taifa – Abeid khamis Bakar ni ya uchochezi, dharau na chuki ambayo ina lengo la kusababisha uvunjifu wa amanina kusababisha mfadhaiko kwa wananchi, serikali inatoa muda wa saa 24 kwa msimamizi na wamiliki wa tovuti hiyo kujieleza kwa maandishi kwanini wasichukuliwe hatua hatua za kisheria na kuomba radhi ndani ya saa 24 kuanzia saa 9:00 alasiri ya leo Februari 24, 2017
Wahariri na wamiliki wa mtandao huo wanatakiwakufika kesho blia kukosa Idara ya habari Maelezo Zanzibar saa 3:00 asubuhi.
Aidha, serikali inavionya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuacha kuchapisha, kuonnyesha na kusambaza taarifa za uongo, uchochezi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa chombo chochote cha habari, mitandao ya kijamii itakayokwenda kinyume na sheria
Imetolewa na :
Hassan Vuai,
Mkurugenzi Idara ya Habari -MAELEZO.
No comments :
Post a Comment