Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 13, 2017

CUF: MAPITIO YA TAARIFA NA MATUKIO MBALIMBALI YA WIKI LEO TAREHE 13 MACHI, 2017!

Image result for cuf images of zanzibar

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 13/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma-CUF Taifa
MAPITIO YA TAARIFA NA MATUKIO MBALIMBALI YA WIKI LEO TAREHE 13 MACHI, 2017
Hii ni mara tano sasa tukikuletea mukhtasari na majumuisho ya mapitio ya taarifa, matukio na misimamo ya Chama juu ya masuala mbalimbali kuhusiana na CUF kwa lengo la kuwajulisha wanachama, viongozi na watanzania kwa ujumla masuala yapi muhimu yanayoendelea ndani ya CUF na kuwekana sawa kwa kuwapa “Updates” na kusahihisha taarifa za upotoshwaji/propaganda chafu dhidi ya Chama (CUF Weekly Report).
KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA WIKI HII INAPENDA KUWALETEA TAARIFA ZIFUATAZO:
1. CUF YAPATA USHINDI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO WILAYA YA LINDI MJINI;
Wananchi wa wilaya ya Lindi Mjini wamewadhihirishia watanzania kuwa wanataka mabadiliko, jana tarehe 12/3/2017 chama cha CUF kimefanikiwa kushinda mitaa yote saba 7 iliyofanya Uchaguzi. Hapo awali CUF ilikuwa inaongoza mitaa 3 na CCM mitaa 4. Mitaa hiyo ni Sabasaba, Mnubi, Ndoro, Migombani, Rahaleo “B, Tulieni, na Narunyu. Pongezi kwa timu nzima iliyofanikisha ushindi huu ikiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya Mhe, Salum Baruwani, Kassim Fundi (Mratibu) pamoja na viongozi wote wa Kamati ya Utendaji wilaya. Pia Mhe. Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, Mhe. Diwani Kassim Mshamu, Mhe. Mohamed Mluya na madiwani wengine wote walioshiriki kufanikisha ushindi huu wakiwemo wabunge wa mikoa ya kusini wakiongozwa na Mhe. Hamidu Bobali. Ushindi katika uchaguzi huu unatoa salamu kwa wale wote wenye fikra mgando za kutotaka mashirikiano ya vyama katika kupambana na CCM.
Viongozi na wanachama wa CUF wilaya za Lindi walishampiga marufuku Lipumba na genge lake kujihusisha na siasa kwenye wilaya zao na hata pale alipojaribu wilayani Ruangwa alijikuta akizomewa na kufungiwa ofisi. Uchaguzi huu wa marudio ulisimamiwa na Viongozi wa CUF Taasisi ikishirikiana na vyama vya UKAWA.
Ukilinganisha na uchaguzi wa marudio wa madiwani uliofanyika mwezi Januari katika kata 20, Lipumba na timu yake ya Msajili walisimamisha wagombea takribani 16 wakaingiza sehemu ya zile milioni 369 za wizi na kuambulia kata SIFURI. Watanzania wanapaswa kuendelea kutambua kuwa Lipumba na wahuni wake wamekuwa wakihujumu mafanikio CUF.
2. KUHUSU MASHAURI/KESI ZINAZOENDELEA MAHAKAMANI;
Mpaka sasa Bodi ya wadhamini ya CUF inaendelea kusimamia mashauri matatu yanayoendelea mahakamani kama ifuatavyo;
A. Shauri la madai (Miscellaneous Cause No. 3/2017) Mahakama Kuu ya Tanzania-Main Registry kuhusiana na wizi wa fedha za ruzuku na madai ya kurejeshwa fedha zote katika akaunti halali ya Chama, bado halijapangiwa Jaji na tarehe ya kusikilizwa.
B. Shauri Namba 23/2016 dhidi ya Msajili, Mwanasheria Mkuu wa serikali, Lipumba na wenzake limepangwa kutajwa tarehe 22/3/2017 na bado Jaji Kihiyo hajatoa nyaraka zinazohitajika ili Bodi ya Wadhamini kupitia kwa mawakili wake itize azma ya kuomba REVISION.
C. Pia kuna shauri la madai Mahakama ya Kisutu limepangwa kusikilizwa tarehe 21/3/2017 dhidi ya Magdalena Sakaya na wenzake. Tutaendelea kuwajulisha hatua mbalimbali zitakazofikiwa juu ya mashauri hayo.
3. LIPUMBA NA KAMATI YA UTENDAJI BANDIA ‘FAKE’
Jana tarehe 12/3/2017 Lipumba alizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa za upotoshaji juu ya madai ya wazanzibari kutaka Muungano wa haki na usawa kwa pande zote mbili eti kwa kufanya hivyo wanataka kuuvunja Muuungano. Lipumba anaendelea kujidhihirisha wazi kuwa yeye ni wakala wa kutetea ajenda za CCM kuitawala Zanzibar kwa mabavu bila ya kuzingatia Muungano unaotokana na ridhaa ya wananchi. Lipumba ameshindwa kueleza ni Baraza lipi lililokataa Sera ya kudai Mamlaka kamili ya wazanzibari kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015? Maelezo ya kina kuhusu ukibaraka na kutumika kwake ‘Mubashara’ yametolewa vizuri na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui tarehe 8/3/2017 katika Mkutano na waandishi wa habari. Wanachama, wapenzi wa CUF na watanzania wote wapenda mabadiliko tuendelee kumpuuza na kuzipuuza propaganda za Lipumba na wahuni wenzake. CUF kama taasisi Imara itashinda hila na njama ovu dhidi yake na wale wote wenye dhamira mbaya dhidi ya CUF. Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi Taifa Mhe. Julius Mtatiro na viongozi wengine wa CUF wapo tayari kufanya mjadala na mdahalo na yeyote juu ya masuala yote yanayoendelea ndani ya CUF na juu ya sera za CUF, Muungano na masuala mengine. Lipumba hana uhalali (Legitimacy) ya kuwa kiongozi wa CUF. Hakubaliki, na ameshafukuzwa uanachama.
Uongozi wa Chama Taifa unaotambulika na kuthibitishwa na Baraza Kuu la uongozi Taifa ni; Kamati Uongozi Taifa inaongozwa wajumbe watatu (3) na Mwenyekiti wake Mhe. Julius Mtatiro, Saverina Mwijage (MB), na Katani Ahmed Katani (MB)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa wanaotambuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ni
1. Maalim Seif Sharif Hamad -Mwenyekiti
2. Joran Lwehabura Bashange -Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi
3. Nassor Ahmed Mazrui -Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar Zanzibar
4. Abdallah Khamis – Naibu Mkurugenzi wa fedha na Uchumi
5. Mustafa Wandwi -Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
6. Yussuf Salim – Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama.
7. Omar Ali Shehe- Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi
8. Shaweji Mketo – Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi
9. Ismail Jussa Ladhu -Mkurugenzi wa mambo ya nje na Mahusiano ya Kimataifa.
10. Abdallah Mtolea – Naibu Mkurugenzi wa mambo ya nje na mahusiano ya Kimataifa
11. Salim Bimani – Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
12. Mbarala Maharagande – Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
13. Kulthum Mchuchuri -Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.
14. Pavu Abdallah – Naibu Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.
15. Mahmoud Ali Mahinda, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana Taifa-JUVICUF
16. Fatuma Kalembo- Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake Taifa-JUKECUF
CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI
HAKI SAWA KWA WOTE
———————————————-
MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577

No comments :

Post a Comment