*1_Usizungumze kwa ukali (3:159)*
*2_Jizuie na hasira (3:134)*
*3_Kuwa mwema kwa wengine (4:36)*
*4_Usiwe mwenye kiburi(7:13)*
*5_Samehe wanaokukosea (7:199)*
*6_Zungumza na watu kwa upole (20:44)*
*7_Shusha sauti yako (31:19)*
*8_ Usiwakejeli wengine (49:11)*
*9_Watendee wema wazazi wako (17:23)*
*10_Usiseme maneno ya kuwakosea adabu wazazi wako (17:23)*
*11_Usiingie chumba cha wazazi wako bila kuomba idhini (24:58)*
*12_Andikishianeni mnapokopeshana (2:282)*
*13_Usifuate rai ya yeyote kibubusa (2:170)*
*14_Muongezee unayemdai muda wa kulipa deni kama ana hali ngumu
(2:280)*
*15_Usile riba (2:275)*
*16_Usijihusishe na rushwa (2:188)*
*17_Usivunje ahadi (2:177)*
*18_Tunza amana (2:283)*
*19_Usiufiche ukweli unaoujua (2:42)*
*20_Wahukumu watu kwa haki (4:58)*
*21_Simamia haki (4:135)*
*22_Mali za marehemu zigawiwe kwa warithi wao (4:7)*
*23_Wanawake pia wana haki yakurithi (4:7)*
*24_Usile Mali ya yatima (4:10)*
*25_Watunze yatima (2:220)*
*26_Msiliane Mali zenu kwa dhuluma (4:29)*
*27_Patanisheni miongoni mwa wanaogombana (49:9)*
*28_Jiepushe nakuwajengea watu Dhana mbaya (49:12)*
*29_Msipelelezane na msisengenyane (2:283)*
*30_Msipelelezane au msisengenyane (49:12)*
*31_Toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu (56:7)*
*32_Jihimizeni kuwalisha maskini (107:7)*
*33_Watafuteni wenye kuhitaji muwasaidie (2:283)*
*34_Usitumie ovyo pesa zako (17:29)*
*35_Msiharibu sadaka zenu kwa masimulizi (2:264)*
*36_Wakirimu wageni (51:26)*
*37_Waamrishe watu kutenda mema baada ya wewe mwenyewe kuyatenda (2:44)*
*38_Msifanye uharibifu katika Ardhi (2:60)*
*39_Msiwazue watu kuingia misikitini (2:114)*
*40_Piganeni na wale wanaowapigeni tu (2:190)*
*Pendelea upatapo Msg ya Dini kama hii mtumie Mwenzio, hii ni sadaka Jariya yako na Waislam Wenzako*
No comments :
Post a Comment