Hiang ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.
Amesema nchi hiyo itazidisha uhusiano katika sekta za usafirishaji, uwekezaji, afya na biashara pamoja na kubadilishana utaalamu.
Hiang amesema wameona umuhimu wa kuwapo ushirikiano katika kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa viongozi.
Dk Shein amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Singapore na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwamo Zanzibar kwa kipindi kirefu.
Wakati huohuo, Dk Shein amefanya mazungumzo na mabalozi wa Tanzania walioteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais John Magufuli.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu mjini Zanzibar. Miongoni mwa mabalozi hao ni Pindi Chana anayekwenda nchini Kenya, Abdalla Kilima (Oman), Joseph Sokoine (Ubelgiji), Silima Kombo Haji (Sudan), Fatma Rajab ( Qatar), Batilda Masuka (Korea) na Grace Mgovano (Uganda).
Dk Shein amewapongeza kupata uteuzi huo kutokana na sifa walizonazo katika utendaji wao.

No comments :
Post a Comment