Rais Donald Trump atazungumza na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu.
Mazungumzo yao yatakuwa ya kwanza tangu rais huyo wa Marekani apate ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa jana.
Uhuru Kenyatta atakuwa rais wa nne wa Afrika kuzungumza na rais huyo kutoka taifa lenye uwezo mkubwa duniani.
Kati ya maraisa wa Afrika aliozungumza nao kwa njia ya simu ni rais wa Misri Abdel Fatah al Sisi, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Miongoni mwa maswala wanayotarajiwa kugusia ni swala la usalama ,Somalia na ukame unaendelea kukumba eneo zima la Afrika mashariki.
No comments :
Post a Comment