Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salumna anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelezo kwa watumishi wa Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments :
Post a Comment