Licha ya serikali mkoani Pwani kuahidi kutoa huduma za maziko ikiwemo majeneza mawili gari na chakula jamii ya wafugaji Wabarbaig wamegoma kuzika miili ya ndugu zao wawili kwa zaidi ya siku tano sasa hadi waziri wa mambo ya ndani na wa mifugo na kilimo watakapokwenda kijiji cha Kidomole relini Bagamoyo kueleza ufumbuzi juu ya matatizo yanayowakabili ikiwa ni pamoja na mauaji wanayodai yanafanywa na polisi kwa kisingizio cha opereseheni ondoa mifugo.
Hali hiyo imeibuka mara baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani injinia Evarist Ndikilo kuzungumza na wazee viongozi wa jamii hiyo ya wafugaji akiwaomba iwaombe jamii hiyo ikubali kuzika miili ya marehemu ndugu zao kabla ya mambo mengine.
Wakitoa msimamo wao saa chache baada ya kuelezwa kilichojiri katika mkutano huo ambao jamii hiyo ilikaa mbali wakati mkutano unaendelea wamepinga amri ya mkuu wa mkoa ya kuwataka kutawanyika katika eneo hilo na kusisitiza kuwa hawatazika.
Mauaji hayo yametokea siku ya jumanne ambapo ndugu wawili wa tumbomoja Saimba Kambarelega na Rumay Lazaro Kambarelega walifariki wakidaiwa kupigwa risasi na askari polisi Bagamoyo katika vurugu zilizotokana na wafugaji hao kuzuia mifugo yao isipelekwe kituoni kabla haijahesabiwa ambapo marehemu saimba ameacha wake wawili mmoja akiwa na kichanga kinachonyonya na mwingine anadaiwa ni mjamzito.
No comments :
Post a Comment