Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu akiwemo Keneth Nhizi (41), Venance Chisumuni, (43) wakazi wa Ng’hong’honha na Augustino Mlowa (27), mkazi wa Pushipark wilayani Musoma mkoani Mara ambaye ni Ofisa Ardhi wilayani Musoma kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.
Kamanda Mambosasa mkoani humo, Lazaro Mambosasa alitoa onyo kwa wale wote wanaotaka kutumia vibaya fursa ya makao makuu kuhamia Dodoma, kama mwanya wa kufanya vitendo vya kihalifu, ikiwa ni pamoja na utapeli wa viwanja kwa kutambua kuwa wageni wana uhitaji wa ardhi waache mara moja.
Alisema “Hakuna mhalifu atayefanya uhalifu Dodoma na kuwa salama, lazima atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.”
Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
No comments :
Post a Comment