Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 6, 2017

Mwenyekiti CUF agoma kuachia madaraka!


LICHA ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mdeme kutangaza kumsimamisha uongozi wa Mwenyekiti wa mtaa wa Malimwa Kusini, Ismail Seifu (CUF), ametangaza kutokabidhi ofisi ya mtaa kama alivyoagizwa na DC,
Christina Mdeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
Seifu amesema kitendo cha mkuu wa wilaya kumsimamisha nafasi hiyo haina maana yoyote na hatambui suala hilo kwani yeye alichaguliwa na waananchi na siyo mkuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya aliitisha mkutano wa adhara kwa maelezo kuwa wananchi walimpelekea tuhuma tano ambazo zilikuwa zikimkabili mwenyekiti huyo jambo ambalo amesema siyo tuhuma za wananchi bali ni tuhuma za kutengenezwa kamati yake ya utendaji ambao aliwasimamisha.

Akizungumza na waandishi wa habari Seifu, amesema licha ya mkuu wa wilaya kufanya utenguzi wa uongozi wake bado hatambui jambo hilo kwani waotakiwa kumwondoa ni wananchi waliompigia kura.
Seifu amesema wakati wa uongozi wake alihakikisha anapambana katika kukwamua maendeleo huku akiwa ameokoa zaidi ya Sh milioni nne za mradi wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF ambazo zilikuwa zikilipwa katika kaya hewa zaidi ya kumi.

Awali kabla ya kusimamishwa uongozi kwa kutangaziwa tuhuma tano zilizomkabili Seifu amesema katika uongozi wake hakupendezwa na tabia ya baadhi ya viongozi kukwamisha maendeleo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa inasikitishwa na tabia ya viongozi hao kukwamisha maendeleo ya mtaa huo kwa kutosikiliza matatizo ambayo wanapelekewa.

Amesema licha ya kujitahidi kuhakikisha mtaa huo unapata maendeleo makubwa lakini bado kuna mambo ambayo viongozi wa Manispaa na wilaya wanashindwa kuyatolea maamuzi.

Seifu amesema analazimika kusema hivyo kutokana na kuomba wakaguzi wa milioni kumi ambao ulifanyika huku kukiwa na mapungufu ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti huyo amesema mbali na kuomba wakaguzi lakini bado ameweza kuokoa kiasi cha Sh. milioni nne ambazo zilikuwa zikitolewa katika kaya masikini kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kaya masikini.

Amesema katika uongozi uliopita zaidi ya kaya kumi katika mtaa wa Mlimwa Kusini zilikuwa kaya hewa ambazo zilikuwa zikipokea mradi wa TASAF na taarifa hizo zipo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Mtaa wa Mlimwa kusini hunaongozwa na mwenyekiti kutoka katika muungano wa vyama vinavyounda Ukawa kupitia CUF ambapo mtaa huo ni makazi ya Waziri Mkuu.

“Wapo wanasiasa ambao wamekuwa hawataki maendeleo na badala yake wanaingiza mambo ya siasa katika kazi, mtaa huu unaongozwa na CUF lakini wapo watu ambao wanatamani kuangusha utawala uliopo,” amesema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wao viongozi wa Manispaa pamoja na wilaya hawakuweza kutoa ufafanuzi wa jambo lolote kuhusiana na alichokisema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilimwandikia barua Kumb.Na.AB.380/507/01/17 ya kumtaka mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kutoa taarifa ya ukaguzi uliofanyika katika mtaa wa Mlimwa Kusini.

No comments :

Post a Comment