Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 5, 2017

UTAFITI; Ulaji wa karanga ni kinga dhidi ya magonjwa yafuatayo!


Ulaji wa karanga una faida nyingi hasa pale binadamu anazipozitumia mara kwa mara. Na tafiti mbalimbali zinaonesha ya kwamba ulaji wa karanga huweza kuzuia au kutibu magonjwa yafuatayo:

1. Ulaji wa karanga ni kinga dhidi ya magonjwa ya saratani tumbo.
Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya ‘folic acid’, ‘phytosterols’, ‘phytic acid’ (inositol hexaphosphate) na resveratrol’ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga, hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume!

2. Magonjwa ya moyo.
Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya ‘monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Magonjwa ya moyo kama vile shinikizo la damu.

Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ‘Journal of Nutrition’ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.

3. Ulaji wa karanga ni kichecheo cha kuongeza  nguvu za kiume.
Uwepo wa mafuta yanayopatikana katika karanga, ni tiba tosha dhidi ya uongezaji wa nguvu za kiume kwa wanaume ambao wanasumbuliwa na tatizo hilo.

4. Utumiaji wa karanga ni kinga dhidi ya kiharusi( stroke).
Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au ‘stroke’, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu. Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya ‘Resveratrol’ ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine).

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

Unachotakiwa kufanya ni;
Hakikisha unakula karanga hizi walau mara mbili au tatu kwa wiki ili kuweza kujikinga dhidi ya magonkwa niliyoyaorodhesha hapo juu. Aidha unashauriwa kula karanga hizi zikiwa katika hali ya ubichi kwani tafiti zinaonesha ndizo zenye vitamini sana.

No comments :

Post a Comment