Lema: Tanzania ya viwanda hamuiwezi
Godbless Lema
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema amefunguka na kusema serikali ya awamu ya tano haiwezi kuibadili Tanzania na kuwa nchi ya viwanda kwa sababu fedha zilizopelekwa katika sekta hiyo ni ndogo.
Mbali na hilo Mbunge huyo aligusia pia suala la maji na kusema maji ni hitaji muhimu kwa kila binadamu hivyo serikali ingeweza kuona hiyo fursa na kutengeneza miundombinu mizuri ili ijipatie pesa kupitia maji.
"Maji ni biashara Mh. Mwenyekiti najiuliza kwanini nchii hii haijawahi kuona maji ni biashara, tena maji ni biashara ambayo haihitaji matangazo sababu kila mtu anahitaji maji mahitaji namba moja ya binadamu anayeishi ni maji, mmeshindwa kutengeneza mipira, mmeshindwa kutengeneza miundombinu mizuri na kuweka mita ili serikali iweze kukusanya fedha kutoka kwenye maji, kama hatujaweza kuona kuwa maji ni biashara cherehani nne lazima zitakuwa ni viwanda" alisisitiza Lema
No comments :
Post a Comment