Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai aliyefiwa na Mama yake Mzazi Bibi Mwanaisha Hassan Vuai aliyezikwa kijijini kwao Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Bibi Mwanaisha Hassan Vuai katika Msikiti wa Ijumaa Bwejuu aliyefariki Dunia jana katika Hospitali ya Global alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kusini Unguja Nd. Ramadhan Abdullah Ali wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar hapo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Ali Idd akipokelewa na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara baada ya kuwasili katika mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, huko kijijini kwao Bwejuu.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
Baadhi ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
Matukio tofauti ya kubebwa kwa maiti inapotolewa msikiti hadi sehemu ya kaburi ilipofanyiwa mazishi.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd. Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).
No comments :
Post a Comment