Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, May 21, 2017

Balozi Seif Azungumza na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme wa Jordan!



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akisailiana n a Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Kemisk Mjini Amman Nchini Jordan.Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Baishar, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mjini Amma Nchini Jordan.
Bwana Rami Al – Qusus Kushoto akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk Nchini Jordan.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali wa Pili kutoka Kulia akifafanua jambo wakati Ujumbe wa Viongozi wa Tanzania ulipofanya mazungumzo na Ujumbe wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan.Kushoto yaBalozi Amina ni Balozi wa Tanzania Ukanda wa Mashariki ya Kati Balozi Mohamed Haji Hamza, kulia ya Balozi Amina ni Balozi Seif Ali Iddi, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus pamoja na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammouri.
Balolzi Seif kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan na ule wake uliotoka Tanzania kushiriki Jukwaa la Dunia la Uchumi Nchini Jordan.Kulia ya Balozi Seif ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus pamoja na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammouri.Kushoto ya Balozi Seif ni:- Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Balozi wa Tanzania Ukanda wa Mashariki ya Kati Balozi Mohamed Haji Hamza.
Balozi Seif Kulia akiagana na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al –Qusus na anayeshuhudia wa kwanza kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammouri.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na. Othman Khamis OMPR.A 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameushauri na kuuomba Uongozi wa Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan kufikiria namna unavyoweza kusaidia Taaluma na hata uwezeshaji mifuko ya Tanzania ili iweze kufanikiwa vyema kiutendaji kama ulivyopiga hatua kubwa ya maendeleo Mfuko huo.

Balozi Seif alitoa ushauri na ombi hilo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan hapo katika moja ya Kumbi za Mikutano ya Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk Mjini Amman akiwa Nchini humo kushiriki Jukwaa la Dunia la Uchumi akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Alisema mifuko mingi iliyoanzishwa Nchini Tanzania imekuwa ikikabiliwa na ufinyu wa Taaluma na hata nguvu za kifedha zinazoweza kuiendesha kwa umakini zaidi hali ambayo baadhi yake ikishindwa kufanyakazi na kudumaa kabisa kiutendaji.

Balozi Seif alisema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi tofauti zikiwemo zile za Kiraia na hata za Mataifa ya kigeni zimekuwa zikitoa muongozo wa namna ya Jamii inavyoweza kuendesha miradi yao kwa kujikimu Kimaisha na kupunguza ukali wa Maisha ikisaidiwa na Mifuko iliyopo lakini bado nguvu za kujitegemea kwa Jamii hiyo zinaonekana kusua sua.

Aliualika Uongozi huo wa Mfuko wa Mafalme Abdulla wa Pili wa Jordan kufika Tanzania kujionea Mifuko iliyopo jambo ambalo kwa mtazamo huo wanaweza kuata picha halisi na ikiwezekana Taaluma na maarifa uliyonayo watendaji wake unaweza kuona jinsi gani unaweza kusaidia.

Balozi Seif alisema ipo mifuko ya Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF}, Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi iliyoanzishwa kwa lengo mahsusi la kusaidia Jamii kupambana na ukali wa maisha lakini bado Jamii ya wananchi walio wengi wanaendelea kukabiliwa na maisha duni kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Mifuko hiyo isiyoweza kukidhi mahitaji ya Watu wote.

Alieleza kwamba Serikali zote mbili zilizopo Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa na mipango mbali mbali iliyoanzishwa kama Mifuko ya kujitegemea ili kusaidia Wananchi hasa Vijana kuweza kupata njia zitakazowasaidia kujiendesha Kimaisha.

Alisema njia hizo ni mbadala badala ya kusubiri kutegemea ajira za
Taasisi za Umma ambazo kwa sasa zimepunguwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kukua kwa Teknolojia ya kisasa inayotoa fursa kwa fanyakazi wachache kuwajibika kwa kutumia mfumo huo.

Naye Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali alisema licha ya Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan kutoa huduma kwa Wananchi wa ndani ya Jordan pekee lakini bado una nafasi ya kuangalia jinsi unavyoweza kusaidia Tanzania katika misingi ya kudumisha ushirikiano na uhusiano ulipo kati na Mataifa hayo mawili.  

Balozi Amina alisema uhusiano wa Kihistoria unaoendelea kuunganisha Jordan na Tanzania unaweza pia ukatumika kusaidia uanzishaji wa miradi ya pamoja itakayoweza kustawisha zaidi Wananchi wa pande hizo mbili rafiki.

Mapema Mtendaji Kuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus aliueleza Ujumbe wa Tanzania kwamba Mfuko huo uliasisiwa na kupewa nguvu za kiuwezeshaji kutoka kwa Kiongozi huyo ili usaidie Jamii katika mipango wanayojipangia ya Maendeleo.

Bwana Al – Qusus alisema Mfuko huo ambao kwa sasa unajitegemea wenyewe bila ya kupata msaada au ruzuku kutoka sehemu nyengine yoyote unaendelea kutoa Mikopo, kusaidia miradi inayoanzishwa na Vijana, Maendeleo ya Uchumi, Kilimo pamoja na Utalii.

Alisema misaada hiyo inakwenda sambamba na ile ya ustawi wa jamii kwa kuwajengea uwezo zaidi Wanawake ambao ndio wahimili wakubwa wanaotegemewa na familia na Taifa mahali popote pale.

Mtendaji Kuu huyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan alifahamisha kwamba katika mbinu za kuujengea uwezo zaidi wa kiutendaji Mfuko huo, Uongozi wake umeshafungua Matawi yasiyopungua 13 katika maeneo mbali mbali ya Jordan ikiwemo pia Saudi Arabia na Oman.

Aliuhakikishia Ujumbe wa Tanzania kwamba Jordan kupitia Mfuko huo wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili bado una nafasi ya kushirikiana na Tanzania katika uanzishwaji wa miradi ya maendeleo inayoweza kusaidia Jamii ya pande zote mbili rafiki.

No comments :

Post a Comment