Jeshi la polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa hospiltalini lakini madaktari wamesema walipompokea mwanamke huyo kutoka kwa polisi akiwa tayari amefariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Haji Khamisi Haji amesema waliamua kumpelaka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu.
Daktari aliyemfanyanyia uchunguzi marehemu huyo khalifan said salum amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi akiwa tayari ameshafariki dunia.
Amesema wakati anaendelea kumpima marehemu hyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hiyo kuchukuwa sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hiyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya michewi amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la polisi.
/ Pemba News
Earlier report from Pemba:http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2017/05/baba-na-mama-watuhumiwa-kuua-mtoto-wao.html
No comments :
Post a Comment