Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.
Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam.
Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.
Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.
“Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.
No comments :
Post a Comment