dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 20, 2017

Rais Magufuli akabidhi rasmi uenyekiti EAC kwa Rais Museveni!

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.

Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.

Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.

“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.

Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.

No comments :

Post a Comment