Serikali ya mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku uuzaji wa vyakula katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na utaratibu wa kufuturishana ili kuepuka maradhi ya ugonjwa wa kipindupindu.
Cholera bacteria
Wakati mvua za masika zikishika kasi na kuziathiri nyumba kadhaa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema watu 23 wamegundulika kwa na ugonjwa wa kipindupindu.Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Waziri wa Elimu, Riziki Pembe Juma amesema miongoni mwa watu hao yumo mtoto wa miezi mitatu na mzee mwenye miaka 75.
Riziki amesema waliobainika kuathirika na maradhi hayo ni wananchi kutoka wilaya za Mjini, Magharibi A, Magharibi B na Kaskazini A kwa upande wa Unguja na wilaya za Micheweni na Wete kisiwani Pemba.
Amesema kambi imefunguliwa Chumbuni na tathmini ya madaktari inaonyesha wagonjwa hao wameathiriwa kutokana na mazingira kuwa machafu kutokana na mvua iliyosababisha baadhi ya nyumba kuzungukwa na maji.
Kutokana na hilo, Wizara ya Afya imepiga marufuku uuzaji wa vyakula usiofuata sheria na kwamba, kwa kushirikiana na taasisi zingine itatoa elimu kwa jamii, kutoa dawa na maji kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Afya, Dk Mohamed Dahoma amesema ni wajibu wa wazazi na walimu kuwalinda watoto ili wasiambukizwe maradhi hayo.
No comments :
Post a Comment