dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 18, 2017

Mchungaji atiwa mbaroni baada ya waumini wake aliokuwa akiwabatiza mtoni kufariki!


Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mchungaji baada ya waumini wake wawili kufa maji alipokuwa akiwafanyia ubatizo kwenye mto Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi, watu hao walizidiwa na nguvu kubwa ya mkondo wa maji ya mto Ungwasi uliopo wilayani Rombo.

Mpaka sasa bado haijajulikana Mchungaji huyo pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Shalom waliokuwa wanaendelea na zoezi hilo walivyookoka. Hawa ni waumini  wa Kanisa lililopo wilayani hapo.

Makanisa mengi barani Afrika yanatumia njia hii ya kubatiza waumini mtoni badala ya makanisani kwakuwa kwa kufanya hivyo, ni sawa na ubatizo aliofanyiwa Yesu Kristo katika Mto Jordan.

Shuguli hii ya ubatizo kwa waumini wa madhehebu ya dini ya Kikristo huashiria kufutiwa kwa madhambi na kuanza kwa maisha mapya.

No comments :

Post a Comment