Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Friday, July 28, 2017

Msukuma nurusa amchape makonde Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji!


MBUNGE wa jimbo la Geita Vijijini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Joseph Kasheku Musukuma nurusa amchape makonde hadharani Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome Wilayani humo Thomas Halila, muda mfupi baada ya Mbunge huyo kuongoza mamia ya wananchi wa kijiji hicho kungíoa vigingi vilivyowekwa kwenye mipaka ya eneo la Serikali ya kijiji hicho linalodaiwa limeuzwa kinyemela Tsh. Million sita (600,000.),na mwenyekiti Halila, wakishirikiana na mtendaji wa kijiji hicho Charles Mbilingi kwa kutumia Muhtasari wa majina na saini hewa za wakazi wa kijiji hicho.
Hatua ya Mbunge huyo kuongoza,mamia ya wananchi wa kijiji hicho kisha kungíoa vingingi kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa hekali moja na nusu ilikuja baada ya malalamiko ya wananchi hao kudai kutoshirikishwa na kwamba majina yaliyomo kwenye muhtasari wa kikao hicho na hata saini ni za kughushi hali iliyomlazimu Mbunge huyo kusoma jina moja baada ya jingine ili kubaini janja nyani iliyofanywa na mwenyekiti pamoja na mtendaji huyo.

Ambapo iligundulika,mhtasari uliotumika kuuza eneo hilo ni wa kughushi kutokana na wananchi hao kukana kushiriki kikao hicho kilichoketi 15/07/2017 kubariki uuzwaji wa eneo hilo mbali na majina yao kusomwa hadharani,huku diwani wa kata hiyo Masumbuko Sembe akigeuka mbogo baada ya jina lake kuwa miongoni mwa yaliyosomwa na Mbunge wao.

Kufuatia udanganyifu huo, Mbunge huyo akalazimika kuongoza wananchi kwenda kungíoa vingingi vilivyowekwa kwenye mipaka ya eneo hilo lililouzwa kwa mtu ambaye hakufahamika kwa majina wala makazi yake,sambamba na kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Deus Seif kuondoka na mtendaji huyo.

No comments :

Post a Comment