Na Omary Mngindo, Mlandizi
MTOTO mwenye miaka miwili na nusu aitwaye KAIRA KIBELA amepotea katika mazingira ya kutatanisha.Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Mlandizi Alhamisi ya Julai 27, majirani wa mtoto huyo walìsema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu ya Julai 23 saa 3 asubuhi wakati mtoto huyo na mwenzake ambao ni mapacha walikuaa katika michezo yao ya kawaida maeneoya nyumbani kwao.
Majirani hao Nassoro Selemani 'Mzee Ndugu' alisema kwamba siku ya tukio watoto hao walikuwa wanacheza kama kawaida yaolakimi ilipofika saa 3 kaa kawaida ya mama yao aliwaita kwa ajili ya kuwapatia uji kwa mshangao alimuona mmoja tu, huku mwingine Kaira asimuone.
"Alipowaita alishangazwa kumuona mmoja pasipokumuoma Kaira, alitoa taarifa kwa majira zake kuhusiana na tukio hilo ambao waliungana kuanza kumtafuta mtoto huyo pasipo mafanikio, wakaenda Kituo cha Polisi cha Mlandizi kutoa taarifa kuhudiana na tukio hilo," alisema Mzee Ndugu.
Kwa upande wake Bi. Zuhura Selemani Mzava alisema kwamba siku ya tukio walipatwa na mshangao kutokana na hali hiyo huku akieleza kwamba kumekuwepo na matukio ya kawaida ya kupotea kwa mtoto lakini anaonekana baadae lakini kwa Kaira imekuwa mtihani mkubwa.
"Hivi tunavyoongea familia ya mtoto imechanganyikiwa kutokana na tukio hili, kila siku wamekuwa watu wa kuhangaika huko na huko wakimtafuta mtoto huyo nasi majrani kwa upande wetu tunajitahidi kutoa taarifa kwa watu mbalimbali lengo likiwa ni kupatikana kwa mtoto huyo," alisema Bi. Zuhura.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kaloleni Kilindo Ahmed Ally alielezea masikitiko yake kufuatia kuwepo kwa tukio hilo ambapo alisema ni la kwanza kutokea kwenye Kitongoji chake huku akieleza Serikali na wakazi wake kwa pamoja wamekuwa pamoja na familia katika kufanikisha upatikanaji wa mtoto huyo.
"Tupo kwenye mthihani mkubwa, sisi viongozi wa Serikali kwa ushirikiano na wananchi tunaungana na familia kumtafuta mtoto huyo, tunachangishana nauli ya kuiwezesha familia kwenda sehemu moja au nyingine ikiwa ni kufanikiwa kumpata mtoto, tunawaomba wa-Tanzania popote watakapomuona mtoto huyo pichani watoe taarifa katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu," alimalizia Kilindo.
No comments :
Post a Comment