dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 28, 2017

Tamasha la 22 la Mzanzibari Lavutia Wananchi wa Zanzibar!


Wasanii wakicheza Ngoma ya Kiluwa wa Kati wa Tamasha la 22 la Mzanzibari lililofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Squar Michezani Zanzibar na kuvutia wananchi wengi waliofika katika viwanja hivyo kujionea jinsi ya ngoma za asili wakati huo zilivyokuwa kivutio cha Utamaduni wa Zanzibar.
Wasanii wakiwa na Mavazi ya Asili ya Zanzibar wakionesha mavazi hayo wakati wa Tamasha la Mzanzibari katika Viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar.
Wasanii wakicheza ngoma ya mwanandege wakati wa Tamasha hilo la 22 la Mzanzibari katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani.
Wasanii wakicheza Ngoma ya beni bati wakati wa Tamasha hilo.
Wananchi wa Zanzibar wakiwa na vifaa vya Asili ya Zanzibar vya uvinyazi wa vyungu.
Jinsi ya matumizi ya zana za uvuvi Wavuvi wakiwa na mapakacha na mipondo ya ngalawa wakirudi bahari wakionesha wakati wa Tamasha hilo vifaa hivyo vilikuwa vikutumika zamani. 
Kinama Mama wakiwa katika vyazi la buibui la ukaya wakiwa na ukili wakisuka wakionesha katika Tamasha hilo la Mzanzibari katika viwanja vya michezani Zanzibar.
Wananchi wa Mkoa wa Kusini wakionesha jinsi ya tukio la asili la mwaka kongwa wakati wa Tamasha hilo jinsi utamaduni huo unavyokuwa kumaliza visasi na kurudi katika upendo baada ya kumalizika sherehe za mwaka kongwa hufanyika kila mwaka katika Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.




Vijana wakionesha utamaduni wa Zikiri wakati wa Tamasha hilo katika viwanja vya Michenzani Zanzibar.


Vijana wakisoma Maulidi ya homu wakati wa maonyesho ya Tamasha la 22 la Mzanzibari.


Vijana wakicheza ngoma ya danedane sare wakati wa Tamasha hilo.

/Mapara

No comments :

Post a Comment