Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. Hii ikiwa ni bado masaa machache kabla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Sehemu ya mawaziri na manaibu waziri wa Tanzania na Uganda wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
Sehemu ya wageni waalikwa wa mataifa mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
Wakuu wa Mikoa wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea kwenye dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli.
Baadhi ya wasanii wa Kizazi kipywa wakiwa kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana kwa mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kwa mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiagwa kwa saluti na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana usiku mwema na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli.
Picha na IKULU
No comments :
Post a Comment