dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 17, 2017

Nyalandu afunguka alichoteta na Lissu Hospital!

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amesema amezungumza na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye ameonyesha uso wa tabasamu, huku akimshukuru Mungu kwa kumruhusu kuwa hai.

Nyalandu katika ukurasa wake wa Facebook ameandika, “Muda mfupi uliopita, nimeonana na Mh. #TunduLissu katika chumba chake Hospitali ya Nairobi na kuzungumza naye kuhusu hali yake na anavyoendelea.”

“Ukweli ni kwamba, ameumizwa vibaya. Imeelezwa kwamba madaktari wanaendelea na hatua kadhaa za matibabu, wakiwa wameanza kwa kumuimarisha (stabilization), ili kuufanya mwili uweze kumudu hatua zaidi za utibabu anazopaswa kufanyiwa,” amesema Nyalandu.Amesema anaamini hatua zaidi na za haraka zitahitajika kumsaidia apate huduma za kitabibu katika ubora na ufanisi uliopo kwa sasa duniani.

“Ni maombi yangu kwetu sote, tuweke pembeni tofauti zetu za kiitikadi, ama mitazamo, tuungane na kushikamana kama Taifa kwa ajili ya kumwomba Mungu anyooshe mkono wake na kumponya,” amesema Nyalandu.

Nyalandu amesema, “Sote tuungane kutoa msaada wa hali na mali kwa kadri ya uhitaji wake. Amani iwe naye!”

Lissu anaendelea na matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.


/ Mwananchi:

1 comment :

  1. Do you need free Facebook Followers?
    Did you know that you can get them AUTOMATICALLY & TOTALLY FOR FREE by registering on You Like Hits?

    ReplyDelete