Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 11, 2017

Rais Kenyatta kumkatia rufaa Mgombea aliyeruhusiwa na Mahakama!

Uhuru Kenyatta amesema anakusudia kukata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu ya kumjumuisha Ekuro Aukot katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa marudio.

Kupitia kwa Mwanasheria wake Tom Macharia, Rais Kenyatta aliiambia Mahakama kuwa anakusudia kwenda kwenye Mahakama ya Rufaa Jumatatu ijayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya maombi katika hukumu ya Mahakama Kuu kumruhusu Dr. Aukot kugombea Urais kutangazwa na Justice John Mativo.Jumatano, Justice Mativo alisema kuwa Dr. Aukot lazima ajumuishwe kwenye uchaguzi wa marudio ambao umepangwa kufanyika October 26, 2017.

Mahakama ilikwenda mbali zaidi kuieleza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kurekebisha katika maandalizi yao na kumjumuisha Dr. Aukot kama mgombea.

No comments :

Post a Comment