dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 6, 2017

Serikali yakanusha Mwenge kuhusika na Masuala ya Siasa!



Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud amesema lengo la kuasisiwa mwenge ni kupambana na maadui mbali mbali wa taifa wakiwemo ujinga, maradhi na umasikini. 

Alisema zipo dhana kwa baadhi ya wananchi kwa kudai kuwa mwenge ni swala la kisiasa huku akieleza ukweli na kuwataka wananchi kutambua kuwa swala la mwenge ni la Serikali na sio Siasa.

Mh. Ayuob aliyasema hayo leo kwenye mkutano maalum na waandishi wa habari Mh. Ayoub amewataka wananchi wote wa mkoa wa mjini magharibi na hasa vijana kuhudhuria kwa wingi katika uzinduzi wa wiki ya vijana ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mnamo tarehe 8/10/2017 ambapo maonyeshesho, midahalo na burudani mbali mbali za vijana zitakuwa zikifanyika.

Oktoba 14, 2017 Itakuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar kufanyika kilele cha mbio za mwenge katika mkoa wa mjini magharibi ambapo Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maghufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi akiongozana na viongozi mbali mbali wa kitaifa.

No comments :

Post a Comment