Hatua ya kiongozi wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga kujitoa kushiriki uchaguzi wa marudio ni mfululizo wa matukio ya vituko katika siku za karibuni kuhusu mgogoro wa kura.
Wakenya wameshuhudia waapigakura wakijitokza kwa idadi kubwa Agosti 8 baada ya kampeni kali zenye mvutano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.
Kuna hofu kwamba kampeni kali zilizojaa hasira zinaweza kusababisha machafuko huku ikiwepo kumbukumbu kwamba zaidi ya watu 1,100 waliuawa katika vurugu zilizochochewa kisiasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Agosti 8 yanampa Kenyatta mwelekeo wa ushindi lakini mara Odinga, ambaye anadai kuna watu walidukua taarifa na kuvuruga matokeo.
Matokeo rasmi yaliyochapishwa Agosti 11 yanampa Kenya ushindi wa asilimia 54.27 ya kura zote na Odinga anapata asilimia 44.74. Maandamano yanaibuka katika maeneo ambayo ni ngome ya Odinga. Machafuko yanaendelea kwa siku kadhaa.
Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNCHR) inasema watu 37 wameuawa kwenye vurugu hizo, wengi wao na polisi.
Mara Odinga anawasilisha malalamiko yake Mahakama ya Juu. Katika hali ya kushtua, majaji wake Septemba Mosi wanatangaza matokeo ya urais ni “batili na hayatambuliwi” na wanaamuru ufanyike wa marudio ndani ya siku 60.
Kwanza tarehe ya uchaguzi huo wa marudio inatangazwa kuwa ni Oktoba 17.
Taarifa ya siri ambayo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inaonyesha wakikiri kuwepo dosar na kushindwa kusimamia vema kura inawekwa hadharani Septemba 7.
Kadri hofu ilivyoongezeka juu ya uwezo wa Kenya kuandaa uchaguzi mwingine wa kura ya rais, kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya OT-Morpho kutoka Ufaransa iliyosambaza vifaa hivyo vya kupigia kura Septemba 18 ikasema haitakuwa tayari kwa muda huo.
Mahakama ya Juu inaweka hadharani maelezo ya kina ya hukumu iliyoishutumu IEBC kwa kushindwa kusimamia vyema uchaguzi. Kisha IEBC inatangaza kwamba imesogeza mbele uchaguzi wa marudio hadi Oktoba 26.
Septemba 23, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Kenya anatoa amri ufanyike uchunguzi juu ya mwenendo wa tume katika suala ya kusimamia kura.
Mwishoni mwa Septemba chama tawala cha Jubilee kinawasilisha bungeni miswada inayolenga kutatua “utata” katika sheria ya uchaguzi.
Nasa wakiongozwa na Odinga wanalaani hatua hiyo kama juhudi za kuingiza baadhi ya mambo “yasiyofuata kanuni na taratibu za sheria” yaliyotajwa na Mahakama ya Juu kuwa yalichangia uchaguzi kufutwa.
Maandamano mengine yanazuka mwanzoni mwa Oktoba huku Odinga akitoa wito kwa wafuasi wake kuishinikiza Serikali kubadili tume ya uchaguzi, na akitishia kuwa hatashiriki katika uchaguzi wa marudio.
Oktoba 10, anatangaza kujiondoa kugombea tena akidai jopo limeshindwa kufanya marekebisho yanayohitajika.
Aidha, anabainisha kuwa hiyo haimaanishi kuwa vita yake imekwisha akiainisha hoja za chama chake anazoamini zitalazimisha maofisa wa uchaguzi kuanzisha upya mchakato wa uchaguzi mpya kuanzia mwanzo.

No comments :
Post a Comment